Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, October 10, 2014

MTOTO WA MIAKA MITATU ABAKWA NA MJOMBA WAKE


KILIMANJARO wakati serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wakihakikisha wanatokomeza kabisa unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo pamoja na wanawake, mkoani Kilimanjaro  matukio ya kubakwa na kulawitiwa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 10, yamezidi kukuwa kwa kasi.

Matukio hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakihusiswa na imani za kishirikina, yamezidi kukua kwa kasi, ambapo yamejidhihirisha baada ya juzi, mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu, kubakwa na mjomba wake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita alisema kuwa, tukio hilo lililotokea Oktoba 8, mwaka 2014 majira ya saa 10:46 jioni, katika kijiji cha Sabuko, Kata ya Mbiriri, tarafa ya Siha wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Kamanda Moita alisema kuwa, Mtoto huyo (jina tunalihifadhi), alibakwa na mjomba wake, aliyetambulika kwa jina la Emmanuel John (16), na kumsababishia maumivu makali sana sehemu za siri.

“Mjomba wake huyo, alifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo, ambapo alikuta wazazi wake hawapo, ndipo alipoamua kufanya tukio hilo la kinyama kwa mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri,” alisema Moita.

Aidha Kamanda Moita alisema kuwa, mara baada ya mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho cha kimyama,  alipata maumivu makali katika sehemu za siri, yaliyomsababishi kukimbizwa katika hospitali ya Kibosho ambapo amelazwa huko kwa matibabu zaidi.

Pia Kamanda Moita alisema kuwa, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani.


Na Paul Wilium,

No comments:

Post a Comment