Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 20, 2014

Mwalimu auwawa kikatili na mwili wake kutupwa kwenye mtaro wa maji machafu

KILIMANJARO mtu mmoja alietambulika kwa jina la Eliuteri Leon Kiwia (45) mkazi wa uru Kimanganuni  na mwalimu wa shule ya ufundi na compuiter Santa Cacilia iliyopo Uru Njari amekutwa amekufa maeneo ya Uru Kimanganuni kata  ya Uru Kusini tarafa ya Hai Mashariki  wilaya ya Moshi Vijijini  mnamo  tarehe  19 octoba mwaka 2014 majira ya 06:15 hrs.

Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kilimanjaro Koka Moita, alisema mtu huyo alikutwa amekufa baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake kutumbukizwa katika mfereji wa maji  pembeni mwa barabara ya lami na watu wasiojulikana.

Alisema baada ya mwili wa marehemu kukaguliwa kwenye eneo la tukio ulikutwa na jeraha kubwa kichwani na  kukutwa na fedha 300,300 pamoja na simu ndogo  ya mkononi aina ya Samsung.

Aidha alisema kuwa chanzo cha mauwaji hakijafahamika na hakuna aliye kamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea kufanyika ili kuwabaini wahusika watukio hilo. >>> "Hadi sasa hajafahamika kama kuna mali yoyote iliyoibiwa na uchunguzi wakina unaendela  juu ya mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kutambua na hatimae kuwakamata wauwaji" alisema Kamanda Moita.

Pia ametoa wito kwa wananchi wote wanaofahamu jambo lolote linaloweza kusaidia kukamatwa kwa watuhumiwa wa tukio hili wasisite  kutoa taarifa  polisi na zitafatiliwa kwa kina ili kuwatia mbaroni wahusika alisema Kamanda Koka.

No comments:

Post a Comment