Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, October 18, 2014

Wazazi na walezi wanaowaozesha watoto kabla ya kuhitimu masomo yao kukiona chamoto

NJOMBE  serikali  imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wazazi na walezi ambao wanawaozesha watoto wa kike wanaohitimu elimu ya msingi na sekondari  badala yakuwaendeleza kimasomo.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya njombe Bi. Sara Dumba  ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya  wasichana ya  Manyunyu iliyoko kata ya Matembwe wilayani humu  Njombe Mashariki.

Aidha Bi. Dumba alisema bado wapo wazazi ambao wanawaozesha watoto badala ya kuwapeleka shule hata kama wamechaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari ama elimu ya juu.

Awali akisoma taarifa fupi ya shule hiyo mkuu wa shule  Bi. Neema Nzowa  alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchakavu wa mabweni na upungufu wa watumishi
.
Nao wanafunzi waliohitimu kidato cha nne waliainisha changamoto zao mbele ya mgeni rasmi kuwa baadi ya wazazi wanashindwa kuchangia chakula na michango mingine jambo ambalo lina walazimu waalimu kuwarudisha wanafunzi majumbani kufwata michango hiyo.

No comments:

Post a Comment