Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, November 13, 2014

Jimbo la katoliki mjini Moshi waamua kujenga shule ya walemavu mchanganyiko

KILIMANJARO jimbo la katoliki la mjini Moshi, wameamua kujenga shule ya walemavu mchanganyiko katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai mkoani Kilimanjaro iliwaweze kusoma katika mazingira rafiki na waweze kupata elimu inayoenda  sambamba na teknolojia  ilikumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na mwanaharakati wa mtandao huu Ofisini kwake  Askofu mkuu wa jimbo katoliki la Moshi Issac Amani, alisema ujenzi wa shule hiyo  ya sekondari ya watoto walemavu mchanganyiko ni  wazo la kanisa hilo, baada ya kuona watoto wengi wenye mahitaji maalumu wakishindwa kuendelea na masomo ya juu.

Alisema kuna watoto wenye ulemavu na wana vipaji mbalimbali na wanapochanguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, wanakutana na changamoto za mazingira yasiyo rafiki ya kusomea na  ukosefu wa waalimu wenye uwezo kitaaluma katika kuwafundisha  watoto wenye ulemavu.

Aidha Askofu Amani ameiomba jamii na taasisi mbalimbali kunga mkono juhudi za ujenzi wa shule hiyo, ili kuwasaidia watoto hao wenye ulemavu waweze kupata elimu nzuri, kama  watoto wasiyo na  ulemavu.

Na kuwakumbusha watu wenye nafasi katika jamii kuwa na  kila mmoja wetu atambue kuwa anawajibu wa kuisaidia jamii hususani yenye ulemavu na siyo kuiachia serikali peke yake.

No comments:

Post a Comment