Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, December 11, 2014

Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni nne na walimu mkoani Kilimanjaro

KILIMANJARO walimu mkoani Kilimanjaro wanaidai serikali zaidi ya bilioni 4 ikiwa ni malimbikizo ya madai mbalimbali ikiwemo malimbikizo ya mishahara ya walimu waliopandishwa madaraja.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa chama cha walimu mkoani Kilimanjaro (CWT) Nathanael Mwandete, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu ofisini kwake jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mwandete alisema mpaka sasa madeni ya walimu wanayoidai serikali yamefikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni nne ambayo yanatokana na malimbikizo ya mishahara, posho za uamisho na malimbikizo ya mishahara baada ya kupandishwa madaraja.

Aidha alisema mpaka sasa serikali imeanza kupunguza kwa kuyalipa madeni hayo kupitia akaunti za mishahara ya walimu kuanzia mwenzi Septemba mwaka huu baada ya jitihada mbalimbali kufanywa na chama hicho.

Alisema walimu wanastahili haki mbalimbali kwa mujibu wa sheria na kanuni za ajira zao na kwamba walimu wengi wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu pasipo kujaliwa na kupewa posho za mazingira magumu jambo ambao limekuwa likiwakatisha tamaa.

Aidha alisema waajiri wamekuwa wakifumbia macho kero za walimu na kuwakatisha tamaa ya kuendelea kufanyakazi haswa ikizingatiwa mazingira yao ya kazi kuendelea kuwa magumu pasipo kupata maslahi kwaajili ya kuendeshea maisha yao ya kila siku.

Mwandele alitoa wito kwa walimu kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za kazi zao pasipo kukata tamaa na kwamba chama hicho kitaendelea kupigania haki za walimu na kuwachukulia hatua za sheria waajiri wote ambao hutumia madaraka yao kuwakandamiza walimu kwa maslahi yao binafsi.

No comments:

Post a Comment