Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, December 11, 2014

Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi imeombwa kuwaandaa wataalamu wa lugha za alama

KILIMANJARO wizara ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi, imeombwa kuwaandaa watalamu wa lugha za alama ili kutofifisha ndoto za wanafunzi wenye ulemavu wa kutokusikia ambao wamekuwa wakishindwa kuendelea na elimu ya sekondari mkoani Kilimanjaro, kutokana na upungufu wa walimu wenye taaluma hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Msandaka viziwi, iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani hapa, Hellen  Kiwelu ambapo amesema kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakifaulu  kuendelea na elimu ya sekondari na hivyo, kushindwa kuendelea na masomo yao.

Bi Kiwelu amesema upungufu wa walimu wenye taaluma ya lugha za alama imeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa Wanafunzi wenye ulemavu wa kutokusikia katika mkoa wa Kilimanajro kwa kukosa walimu wenye taaluma hiyo kutokana na uchache wa walimu na hivyo kusababisha kushindwa kufikia malengo yao ya kitaaluma.

Amesema wanafunzi wenye ulemavu huo, wamekuwa wakiishia kidato cha pili kutokana na kutofaulu mitihani yao kwa kukosa walimu wenye taaluma na hivyo kuiomba wizara ya elimu kuona umuhimu wa kuwaandaa watalamu wa elimu ya lugha za alama ili kuweza kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa BRN.

Kwa upande wao wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia wamesema kuwa wamekuwa wakijisikia kutengwa na jamii kwa kutoweza kuandaliwa utaratibu uliokamilika wa kuendelea na masomo yao kwa idadi ya ufaulu wao ngazi sekondari hata zaidi ya hapo.

Aidha wamesema serikali kushindwa kuwatimizia haki yao ya kupata elimu kikamalifu kumeendelea kuwavunja moyo na hivyo kujikuta ndoto zao zikififishwa jambo ambalo ni kinyume na matarajio yao.

No comments:

Post a Comment