Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, February 12, 2015

Baraza la madiwani la halmashauri ya Rombo lawakalia kooni wazazi wasiotaka kuwalipia watoto karo

KILIMANJARO baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Rombo  mkoani Kilimanjaro limeitaka halmashauri hiyo kuwaburuza mahakamani wazazi wanaopinga kulipa  karo za shule.

Pia baraza hilo limepinga hatua ya baadhi ya wakuu wa shule kuwarudisha nyumbani wanafunzi ambao hawajalipa karo za shule.

Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo Antony Tesha alisema halmashauri haiwezi kuendelea kuwafumbia macho wazazi ambao hawataki kuwasomesha watoto.

Alisema lengo la wilaya hiyo ni kuona halmashauri ikiongoza kwa elimu na sio kuona wanafunzi wakirandaranda barabarani kwa madai ya kurudishwa shule kwa kukosa karo.

Baadhi ya madiwani  Clara Gwandu  na Stanslaus Kimario wakizungumza  katika kikao hicho walidai kuwa baadhi ya wakuu wa shule wamekuwa wakiwarudisha nyumbani wanafunzi na hivyo kutoa nafasi kwa madereva bodaboda kuwalaghai watoto wakike na kujikuta wakijiingiza kwenye
mapenzi.

No comments:

Post a Comment