Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, February 21, 2015

SERIKALI YASIMAMISHA UJENZI WA MAJENGO MAWILI YA GOROFA YANAYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

KILIMANJARO serikali mkoani Kilimanjaro imesimamisha ujenzi wa majengo mawili ya gorofa yaliopo katikati ya mjini wa Moshi kutokana sheria za ujenzi kukiukwa ikiwa ni pamoja na kujengwa chini ya kiwango .

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya kushtukiza ya ukaguzi wa majengo hayo yaliopo katikati ya mji wa Moshi kufuatia kuwepo taarifa za wananchi juu ya ukiukwaji wa sheria za ujenzi wa majengo hayo.

Majengo yaliyokaguliwa ni majengo mawili moja likiwa linajengwa kienyeji bila kuwepo kwa mkandarasi huku jengo jingine likiwa linajengwa na taasisi ya serikali iliyopo chini ya jeshi la kujenga taifa Suma JKT ambapo jengo hilo limeonekana kukiuka taratibu chache ikiwemo wafanyakazi kuto kuvaa vifaa maalumu vya ujenzi.

Gama alisema amechukua uamuazi wa kusimamisha ujenzi wa majengo hayo kutokana na kujengwa chini ya kiwango kulingana na ukaguzi ulifanywa na wataalamu wa ujenzi wa kiwemo wahandisi wa Manispaa na wa mkoa wa Kilimanjaro.

Kutokana na suala hilo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi kumfikisha mahakamani mmiliki wa jengo moja lililopo karibu na uwanja mdogo wa ndege uliopo eneo la Soweto, kutokana na kukiuka tarabu nyingi za ujenzi.

Licha ya kutoa agizo hilo pia ameitaka halmashauri ya manispaa ya Moshi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya gorofa yalipo mjini hapa ili kuzuia ujenzi wa majengo yasiyo kidhi viwango.

Alisema pamoja na jengo moja kujengwa na taasisi ya serikali hataweza kufumbia macho na kuona sheria za ujenzi zinakiukwa na kwamba taasisi za serikali ndizo zinazotakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kufuata sheria na sio kuongoza kuvunja sheria

Akitoa taarifa ya ukaguzi wa jengo la gorofa lililopo karibu na uwanja mdogo wa ndege mjini moshi Mhandisi mkuu sekretarieti ya mkoa ya Kilimanjaro Hashim Kabanda, alisema kulingana na taratibu za ujenzi mmliki wa jengo hilo Gabriel Sambaya, amekiuka taratibu za ujenzi bado zinaendelea kukiukwa.

Alisema moja ya taratibu na sheria za ujenzi zilizo kiukukwa ni Kutokuwa na ubao wa taarifa za mradi, kukosekana kwa taarifa za ujenzi, kutokuwa kwa Mjenzi mkandarasi, kibali cha kuanza ujenzi kutoka manispaa na katika bodi ya wakandarasi.

Aidha alisema taratibu nyingine zilizo kiukwa ni kutokuwepo kwa michoro sahihi iliyo idhinishwa na mamlaka husika na kutokuwepo kwa mhandisi mshauri wa ujenzi .

Alisema ubora wa kazi zilizokamilishwa ni wa mashaka kulingana na vifaa vilivyo tumika ikiwemo ndondo na kwamba jengo kuendelea kutumiwa kama makazi huku ujenzi ukiwa unaendelea ni kosa kisheria jambo ambalo mmiliki wa jengo hilo alikiri kukiukwa kwa tarabibu hizo .

Akizungumzia jengo lillopo karibu na uwanja mdogo wa ndege meneja wa wakala wa majengo mkoani Kilimanjaro Yohana Mashausi, alisema jengo hilo tayari lina ufa na kwamba aina hiyo hujegwa kwa awamu huku malighafi za ujenzi hupimwa ili kuhakiki ubora na viwango jambo ambalo halijafanyika.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya manispaa ya Moshi Martha Kimambo, alisema usimamizi wa majengo hayo husimamiwa na mamlaka mbalimbali na kwamba ili mradi uwe bora ni lazima mwenye mradi kushirikiana vema na idara husika.

No comments:

Post a Comment