Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, February 11, 2015

Ziara ya Raisi Dk. Jakaya Kikwete mkoani Kilimanjaro


Rais, Dk Jakaya Kikwete,  amekiri kuwa bado taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa madaktari, licha ya kuwepo kwa jitihada za dhati zinazofanywa na Serikali yake ya kumaliza tatizo hilo.

Rais Kikwete alibainisha hayo wakati wa ziara yake Mkoani Mkoani Kilimanjaro, ambapo alizindua jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi, pamoja na jengo la kitega uchumi lililojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Steven Kebwe, pamoja na viongozi wa kisiasa, Rais Kikwete alisema kuwa uhaba uliopo nchini wataalamu wa afya  ni mkubwa ukilinganisha na nchi zilizoendelea.

Alisema kuwa kwa sasa daktari moja nchini anahudumia wagonjwa 30,000 hadi 50,000, huku muuguzi mmoja akihudumia hadi wagonjwa 23,000.

Hata hivyo alisema kuwa idadi hiyo ya madaktari na wauguzi ni tofauti kwa nchi za ulaya ambapo nchi nyingi ambazo amekuwa akitembelea daktari mmoja na muuguzi huudumia wagonjwa 300 hadi 500.

Kutokana na changamoto hiyo Rais Kikwete alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuwasomesha madaktari, pamoja na kuongeza vyuo vya wataalamu wa afya.

Alisema jitihada za Serikali zimeanza kuzaa matunda kwa baadhi ya vyuo ikiwemo chuo kikuu cha Dodoma, Muhimbili, ambapo mwaka jana chuo kikuu cha UDOM kilianza wataalamu wa uuguzi ambapo mwaka huu wanatarajia kupata wataalamu wa udaktari.

Kwa upande wa chuo cha Muhimbili Rais alisema wamepanua wigo wa kupokea wanafunzi wa taaluma ya afya kutoka wanafunzi 250 hadi kufika 300 huku Serikali ikiendelea kufungua vyuo vipya vya kufundisha wataalamu wa afya.

Akisoma risala kwa Rais Kikwete, kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi Dk. Endrew Quaker, alisema kuwa hospitali hiyo imekaa kwa zaidi ya miaka mitano bila kuwa na huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

Alisema kukamilika kwa jengo hilo kutapunguza adha kwa akina mama wajawazito, wazee, watoto pamoja na wagonjwa wengine kwenda kwenye hospitali binafsi ambazo wanapata huduma hiyo kwa garama kubwa.

No comments:

Post a Comment