Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, March 8, 2015

Kampeni ya IMETOSHA ya Mdimu kuwavalisha fulana za kampeni Simba na Yanga leo

Watani wa jadi, miamba ya soka Afrika Mashariki na kati Simba Sports club na Young Africans SC kwa dakika chache leo baadae katika uwanja wa taifa jijini Dar,  wataweka upinzani wao pembeni watakapoungana na mamilioni ya waTanzania na dunia nzima kwa ujumla kupinga mauaji ya ndugu zetu albino, pale watakapovaa fulana zenye maneno IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO mara watakapoingia uwanjani kupasha viungo moto (Warm up) Siku ya leo kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali kuanza.
Balozi Henri Mdimu
Wakiongea kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa kamati ya IMETOSHA Bw Masoud Kipanya na Balozi wa kujitolea wa harakati ya Imetosha mwandishi wa habari maarufu Henry Mdimu ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) waliueleza mtandao huu kuwa jana kutwa walikuwa wakimaliza taratibu za kuwasiliana na vilabu husika yaani Simba na Yanga pamoja na shirikisho la soka nchini TFF ili kuweka mambo sawa ambapo timu hizo pamoja na waamuzi wote watavalia fulana zenye maneno IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO, imeelezwa kuwa kila timu itavaa rangi zake za asili ambapo Yanga itavaa fulana za njano zenye maandishi ya kijani na Simba sc watavaa fulana nyeupe zenye maandishi mekundu wakati waamuzi watavaa fulana nyeusi zenye maandishi meupe. Mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom unatarjiwa kuchezwa kesho jioni katika uwanja wa Taifa jijini. 

Mwandishi wa habari hii amevipongeza vilabu hivyo vikongwe nchini Simba na Yanga kwa kuweka upinzani wao pembeni na kuungana na mamilioni ya waTanzania nchi nzima akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh J.M Kikwete kupinga vikali kabisa mauaji manyanyaso na udhalilishwaji wa jamii hiyo ya albino, aidha alipongeza shirikisho la soka nchini TFF kwa kuwezesha jambo hili adhimu kufanyika.

         "MUNGU TUBARIKI TANZANIA"
Toka kushoto Mkala Fundikira(Mjumbe) Henry Mdimu(Balozi) Masoud Kipanya( Mwenyekiti) na Kelvina John( Mjumbe)
Source: Umojahabari Blog

No comments:

Post a Comment