Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, March 14, 2015

Wanafunzi 306 kati ya 1420 waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza hawajaripoti shule



KILIMANJARO wanafunzi  306  kati ya 1420 waliopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 katika shule za sekondari  Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro hawajaripoti shule mpaka sasa.

Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Siha  Abrahamu Kanji, alisema jana kwenye wiki ya maonesho ya Elimu kiwilaya yaliyofanyika katika ukumbi wa [RC] Sanya juu na kukutanisha shule mbalimbali za Sekondari na Msingi za Wilaya hiyo, kwa lengo la kuhamasisha elimu iweze kusonga mbele katika wilaya hiyo.

Kanji alisema kuwa kati ya wanafunzi  waliopangiwa kujiunga katika kidato cha kwanza katika Wilaya hiyo mwaka huu walioripoti ni 1095 tu.

Alisema kuwa kati ya waliopangiwa wasichana walikuwa 806 na wavulana 614, alifafanua kuwa wasichana walioripoti walikua 616 na wavulana 476, ambapo alisema kuwa kwa upande wasioripoti wasichana walikuwa 179 na wavulana 127.

Aidha alisema kuwa wanafunzi ambao hawajaripoti baadhi yao wamekwenda katika shule za binafsi na wengine ambao hawajaripoti kabisa, majina yao yameorozeshwa na kupelekwa katika ofisi za watendaji wa vijiji na kata kwa ajili ya ufuatiliaji.

Kwa upande wake Mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Rashidi Kitambulio alisema kuwa idara ya elimu sekondari imefanikiwa kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 43 ya mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 76 kwa mwaka 2014, hata hivyo idara imeweka malengo ya kufikia asilimia 80 kwa mwaka huu 2015.

Alisema kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa kutoa chakula cha mchana kwa shule zote za sekondari kwa mwaka mzima. Kuanzishwa kwa kidato cha tano na sita katika shule tatu ambazo ni Sanya juu yenye mchepuo wa masomo ya sayansi, Oshara na Magadini zenye michepuo ya masomo ya sanaa.

Idara ya elimu sekondari itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha lengo la utoaji elimu bora katika wilaya hiyo, aidha wanafunzi, wazazi, walimu, viongozi mbalimbali kwa ujumla wanaombwa kutimiza wajibu wao ili kufanikisha malengo ya elimu.

No comments:

Post a Comment