Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, April 4, 2015

Jeshi la Polisi lawaasa raia kusherekea sikukuu ya pasaka kwa amani na utulivu

Image result for alama ya jeshi la polisi Tanzania
DODOMA kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma, kamishina msaidizi mwandamizi ACP David Misime, amewataka wakazi wa mkoa wa huo kusherekea sikukuu ya Pasaka katika hali ya amani na utulivu.
 
Aidha amesema kuwa Polisi haitasita kuwakamata watu watakaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ama aina yoyote ya uvunjaji wa sheria.
 
Kamanda Misime amewaasa wananchi watakaokwenda kusali mkesha wa Pasaka wahakikishe nyumba zao zinabaki na watu kwaajili ya kuangalia usalama wa mali zao.
 
Kamanda Misime amewaonya madereva wa vyombo vya moto kuacha kutumia vilevi katika siku za sikukuu ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.

No comments:

Post a Comment