Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, April 1, 2015

Serikali inatarajia kuajiri watumishi 9,345 mwaka huu

Jengo la Bunge-la Jamhuri ya Muungano wa Tanznia.

DODOMA jumla ya watumishi elfu 9,345 wanatarajiwa kuajiriwa katika kipindi cha mwaka huu.
 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi mheshimiwa Steven Kebwe, amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Temeke mheshimiwa Abas Mtemvu.
 
Katika swali lake mheshimiwa Mtemvu, ametaka kujua hatua ambazo  serikali inazichukua katika kukabiliana na tatizo la ukosefu wa watumishi katika hospitali ya Mwananyamala na Temeke zilizopo jijin Dar-es-salaam.
 
Amesema tayari wamepata kibali cha kuajiri watumishi hao ambapo katika kukabiliana na tatizo hilo mwaka jana waliajiri watumishi elfu 10,129.
 
Amesema katika hospitali za Temeke na Mwananyamala watumishi watapangwa kulingana na maombi ya kibali.

No comments:

Post a Comment