Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, April 7, 2015

Vijana wilayani Siha washauriwa kuachana na unywaji wa pombe za kienyeji



KILIMANJARO vijana wa wilaya Siha, mkoani kilimanjaro, wametakiwa kutafuta mbinu mbalimbali za maendeleo zitakazo wawezesha kujishuhulisha na kujiingizi kipato na kuachana na unywaji wa pombe kupindukia.

Imaelezwa kuwa vijana wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwa ajili ya kunywa pombe badala ya kufanya kazi na kwamba hali hiyo inasababisha wajihusishe na vitendo vinavyo hatarisha maisha yao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Sanya Hoyeee, wilayani Siha, Mkoani Kilimanjaro, Moses Munuo alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusu changamoto zinazokwamisha maendeleo ya vijana katika wilaya hiyo.

Aliwataka vijana kujenga utamaduni wa kufanya kazi na kusoma, badala ya kutumia muda mwingi kunywa pombe na kucheza pool table. Ambapo baada ya kulewa wanajiusisha na vitendo  viovu ikiwamo  ngono na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa kama ukiwepo UKIMWI.

Hivyo kuwaomba  vijana kubadilika na kutumia muda mwingi kufanya matendo mema yanayompendeza mwenyezi Mungu ili waishi kwa amani katika dunia hii.

Pia aliwataka wananchi wilayani humo kupanda miti kwa wingi hasa maeneo yanayowazunguka, alisema asilimia 17 hadi 20 ya mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na ukataji miti na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika nchi zinazoendelea.

Amewaomba wananchi wilayani humo kupanda miti kwa wingi pamoja na ya matunda kuzunguka katika maeneo ya wazi hasa katika kipindi hichi cha mvua.

No comments:

Post a Comment