Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, April 3, 2015

Wazee wenye umri wa miaka 60 walamikia kunyimwa viporo na wake zao


KILIMANJARO wazee wa kijiji cha Losaa, kata ya Masama Magharibi, wilayani Hai, mkoni Kilimanjaro wametoa malalamiko yao kwa uongozi wa wazee wilaya kuhusu kunyimwa kitafunwa(kiporo) asubuhi na wake zao.


Wametoa malalamiko hayo leo katika kikao cha wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea kilicho lenga kuibua changamoto wanazo kutana nazo kwa maisha ya sasa ikiwa ni pamoja na kujadili lishe bora na matibabu kwa Wazee.

Wamesema kuwa zipo changamoto nyingi zinazo wakumba likiwemo la kutokupata kifungua kinywa asubuhi wanacho kiita kiporo, pamoja na chakula chenye virutubisho vizuri kwa wazee ikizingatiwa kuwa wanahitajika kutunzwa na jamii iliyo wazunguka.

“Jamani asanteni kwa kufika leo kijijini kwetu nazungumza kwa masikitiko kuwa huku vijijini tunapata taabu kubwa ya chakula kwani baadhi ya wanawake hawatupi kiporo asubuhi licha ya chakula kuwepo nyumbani jambo ambalo lina tulemaza sisi wazee na Serikali yetu ipo tufanyeje?” alisema na kuhoji mmoja wa wazee hao wa kiume katika kikao hicho.

Waliongeza kuwa wazee kutokupata chakula katika jamii kunawasababishia kuishiwa na nguvu kwa haraka hivyo wazee kuonekana kuwa siyo hazina katika jamii ya leo kutokana na wao kuchoka mapema hivyo kuitaka Serikali kuhakikisha kuwa wazee wanathaminika kwa kupewa chakula bora na matibabu ili wazidi kuwepo na kuwa hazina.

Kwa upande wake katibu wa Wazee Wilaya Shikenaufoo Lema aliwataka wazee hao kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji juu ya masuala ya kunyimwa chakula na wake zao ili waweze kusaidika kwa haraka huku wazee  kwa upande wa wanawake wakihitajika kuonesha upendo kwa familia zao hasa ikionekana wote ni wazee ili kuepuka aibu.

“Naiomba jamii ya watanzania ambao siyo wazee kwa sasa watambue kuwa uzee upo na utakuja kuwakuta hivyo kuwataka waweze kuwa na mapenzi mema kwa jamii ya wazee ili wazee waweze kuwa hazina kwa sasa na baadae.” Alisema Lema.

No comments:

Post a Comment