Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, May 19, 2015

Wafanyabiashara wa soko la Siha kuandamana endapo halmashauri haitarekebisha miundombinu


KILIMANJARO wananchi wa Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro, hususani wale waishio maeneo ya kuzunguka soko la Sanya juu wapo hatarini kupata magojwa ya mlipuko ikiwamo Kipindupindu kutokana na kuuza vyakula katika mazingira hatarishi, kufuatia soko hilo kukithiri kwa uchafu na ubovu wa miundombinu.

Wafanyabiashara wa soko hilo wakiongea na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti bila kutaja majina yao kwa kuhofia usalama wao, Wafanyabiashara hao walisema kuwa wanailalamikia Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa madai ya kutokufanya ukarabati kwani soko hilo linahatarisha afya za wafanyabiashara pamoja na wanunuzi wa vyakula katika soko hilo.

Mmoja wa Wafanyabiashara wa soko hilo alisema kuwa wanapanga vyakula chini tena kwenye tope mazingira ni machafu lakini hawana njia nyingine ya kuendesha maisha zaidi ya uendelea kufanya biashara katika soko hilo, aliongeza kwa kusema Halmashauri inakusanya ushuru kila ifikapo siku ya soko na hawajui fedha hizo zinatumika katika shughuli gan?

Wafanyabiashara hao walisema kuwa, soko hilo ambalo limekuwa likitoa Viazi, Ndizi, Maharage na Maparachichi, na kusambazwa katika masoko mbalimbali nchini ikiwamo jiji la Dar es Salaam, linatakiwa kuwekewa miundombinu imara na mazingira kuwa safi wakati wote.

Ambapo waliseme kuwa miundombinu hiyo ni pamoja na kuwekewa Moramu na mifereji ili kuwezesha Wananchi kupita kwa usalama pia wafanya biashara kufanya biashara zao katika mazingira mazuri hasa kipindi hichi cha mvua za masika, tunaomba marekebisho hayo yafanyuke mapema iwezekanavyo kabla hatujaandamana hadi ofisi ya mkurungenzi.

No comments:

Post a Comment