Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, June 11, 2015

Hii hapa listi ya wanamichezo matajiri duniani, Mayweather ang'ara zaidi


Jarida namba moja kwa masuala ya fedha – Forbes kutoka nchini Marekani limetoa listi ya wanamichezo walioingiza fedha nyingi zaidi duniani katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, na ipo kama ifuatavyo.
  
1. Floyd Mayweather Jr.
Mapato yote: $300 million
Malipo ya Ndondi: $285 million 
Matangazo: $15 million 
Mapato haya ya $300 million kwa mwaka yanavunja rekodi mapato makubwa zaidi aliyowahi kuingiza mwanamichezo yoyote kwa kipindi cha mwaka 1. Rekodi iliyopita ilikuwa ikishikiliwa na Tiger Woods aliyeingiza $115 million mwaka 2008.
 
2. Manny Pacquiao

Mapato ya Jumla: $160 million
Mshahara: $148 million
Matangazo ya Biashara: $12 million
Fedha aliyolipwa Pacquiao $125 million kwenye pambano dhidi ya Mayweather ilikuwa mara nne zaidi ya fedha aliyopata katika pambano lake lilopita dhidi ya Chris Algieri. Mapato mengine yametokana na Nike, Foot Locker, Wonderful Pistachios, na matangazo mengine ya biashara.
 
3. Cristiano Ronaldo
Mapato ya Jumla: $79.6 million
Mshahara/Posho/Bonasi: $52.6 million
Matangazo ya Biashara: $27 million
Akiwa bado anashikiliwa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia Ronaldo ndio mwanasoka anayelipwa fedha nyingi duniani mbele ya mpinzani wake Lionel Messi.

 
 4. Lionel Messi
Mapato ya Jumla: $73.8 million
Mshahara/Posho/Bonasi: $51.8 million
Matangazo: $22 million
Mwishoni mwa mwaka jana Barcelona walimpa Mess mkataba wenye thamani ya $9 million kwa mwaka – ambao unamfanya anaondoka na $50m kwa mwaka.
  5. Roger Federer
Mapato ya Jumla: $67 million
Mshahara: $9 million
Matangazo: $58 million
Pamoja na kutokuwa na mafanikio makubwa uwanjani, lakini Federer, bingwa wa mara 17 wa mataji makubwa ya tennis anaingiza fedha nyingi kutokana na mikataba yake ya kibiashara kama Nike, Rolex na Credit Suisse. Na Mwaka uliopita aliongeza mkataba wake na Mercedes Benz kwa miaka 3.


Credit: Millard Ayo

No comments:

Post a Comment