Pages

Wednesday, June 3, 2015

Idadi ya matukio ya ukatili wa kijinsia yanayoripotiwa katika dawati la jinsia mkoani Kilimanjaro yazidi kuongezeka



KILIMANJARO idadi ya matukio ya ukatili wa kijinsia yanayoripotiwa katika dawati la jinsia mkoani Kilimanjaro  imeongezeka kutokana na wananchi kupata elimu na uelewa wa maswala ya kisheria kupitia  wasaidizi wa kisheria wanaotoa elimu hiyo kwa jamii.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto mkoani Kilimanjarao ASP, Mahija Mhando alipokuwa akifunga mafunzo ya wasaidizi wakisheria  ishirini kutoka katika wilaya ya Moshi mjini lililoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la "Kilimanjaro Women Information Exchange and Consultancy Organization" (KWIECO).
Alisema kuwa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia mkaoani Kilimanjaro ni nyingi kuliko miaka ya nyuma kutokana na elimu inayotolewa na wasaidizi wa kisheria  na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali kama KWIECO ambayo yametoa mwanga mkubwa kwa jamii.
Alisema kuwa wananchi waendelee kutoa taarifa zaidi ili haki iweze kutendeka kwani kwa kukaaa kimya watapoteza haki zao na kuendeleza uovu kwa jamii huku wanaoteseka zaidi ni wanawake na watoto ni lazima swala hili lipigwe vita.
Alisema kuwa jamii inapopata matatizo wasiogope kujitokeza wafuate taratibu zilizopo ili kupata haki zao kwani kwa ushirikiano wa polisi na wananchi ukatili na uovu wote katika jamii utatoweka. Pia amewataka wananchi kutumia elimu waliyoipata kuwaelimisha wengine.
Katibu mkuu wa wasaidizi wa kisheria Wiliya ya Moshi, Justine Laswai alitaka mabaraza ya kata kuwapa ushirikiano wa kutosha kwani jamii imeanza kuwaelewa  umuhimu wa wasaidizi wakisheria  katika maisha yao ya kila siku.
"Mabaraza ya kata yaache kupokea jamvi kutoka kwa wananchi pindi wanapotatua matatizo yao na  watoe huduma hiyo bure ili kila mwanajamii awezekupeleka tatizo lake kwa ajili ya ufumbuzi na ikiwezekana mabaraza hayo yaache kutoa huduma hiyo kwani wasaidizi hao wanatoa huduma hizo bure." alisema
Laswai.
Aliendelea kusema kuwa watendaji na baraza ya kata watoe fursa kwa wasaidizi wa kisheria kwenye mikutano ya hadhara na ya mitaa ili waweze kutoa elimu kwa watu wengi zaidi kuliko kusubiri kongamano au tatizo linapojitokeza.
Kwa upande wake  Afisa Mipango ya KWIECO, Moris Venance alisema msaada wa kisheria ni haki ya kila mmoja hivyo wamejipanga kufikia wananchi wote hasa walio sehemu za pembezoni kwa kupitia makongamano na elimu.

Alisema kuwa kupitia makongamano watatoa mafunzo juu ya maswala ya watoto, ndoa, miradhi na ardhi kwa kupitia wasaidizi wakisheria ili kuwafikia na kuwawezesha wananchi kutokomeza ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment