KILIMANJARO idadi ya matukio ya ukatili wa kijinsia yanayoripotiwa katika dawati la jinsia mkoani Kilimanjaro imeongezeka kutokana na wananchi kupata elimu na uelewa wa maswala ya kisheria kupitia wasaidizi wa kisheria wanaotoa elimu hiyo kwa jamii.
Hayo yalibainishwa na
Mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto mkoani Kilimanjarao ASP, Mahija Mhando
alipokuwa akifunga mafunzo ya wasaidizi wakisheria ishirini kutoka katika wilaya ya Moshi mjini
lililoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la "Kilimanjaro Women Information
Exchange and Consultancy Organization" (KWIECO).
Alisema kuwa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia mkaoani Kilimanjaro ni nyingi kuliko miaka ya nyuma kutokana na elimu inayotolewa
na wasaidizi wa kisheria na mashirika
mengine yasiyo ya kiserikali kama KWIECO ambayo yametoa mwanga mkubwa kwa jamii.
Alisema kuwa wananchi waendelee kutoa taarifa zaidi ili haki
iweze kutendeka kwani kwa kukaaa kimya watapoteza haki zao na kuendeleza uovu
kwa jamii huku wanaoteseka zaidi ni wanawake na watoto ni lazima swala hili
lipigwe vita.
Alisema kuwa jamii inapopata matatizo wasiogope kujitokeza
wafuate taratibu zilizopo ili kupata haki zao kwani kwa ushirikiano wa polisi
na wananchi ukatili na uovu wote katika jamii utatoweka. Pia amewataka wananchi
kutumia elimu waliyoipata kuwaelimisha wengine.
Katibu mkuu wa wasaidizi wa kisheria Wiliya ya Moshi, Justine Laswai alitaka mabaraza ya kata kuwapa
ushirikiano wa kutosha kwani jamii imeanza kuwaelewa umuhimu wa wasaidizi wakisheria katika maisha yao ya kila siku.
"Mabaraza ya kata yaache kupokea jamvi kutoka kwa wananchi
pindi wanapotatua matatizo yao na watoe
huduma hiyo bure ili kila mwanajamii awezekupeleka tatizo lake kwa ajili ya
ufumbuzi na ikiwezekana mabaraza hayo yaache kutoa huduma hiyo kwani wasaidizi
hao wanatoa huduma hizo bure." alisema
Laswai.
Laswai.
Aliendelea kusema kuwa watendaji na baraza ya kata watoe fursa kwa
wasaidizi wa kisheria kwenye mikutano ya hadhara na ya mitaa ili waweze kutoa
elimu kwa watu wengi zaidi kuliko kusubiri kongamano au tatizo linapojitokeza.
Kwa upande wake Afisa
Mipango ya KWIECO, Moris Venance alisema msaada wa kisheria ni haki ya kila
mmoja hivyo wamejipanga kufikia wananchi wote hasa walio sehemu za pembezoni kwa
kupitia makongamano na elimu.
Alisema kuwa kupitia
makongamano watatoa mafunzo juu ya
maswala ya watoto, ndoa, miradhi na ardhi kwa kupitia wasaidizi wakisheria ili
kuwafikia na kuwawezesha wananchi kutokomeza ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment