Katika kuwajengea waendesha bodaboda pamoja na abiria wao mazingira bora na salama, mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra, imeanza kujenga kituo maalumu cha mfano kitakacho gharimu zaidi ya shilingi milioni kumi za Tanzania, kwaajili ya waendesha bodaboda wa manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro .lengo likiwa ni kujenga vituo zaidi ya 100 mkoani Kilimanjaro
Kaimu afisa mfawidhi wa Sumatra mkoani Kilimanjaro Bwana Thadei Mwita, amesema hayo wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga, alipotembelea eneo la stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani panapojengwa kituo cha mfano, cha waendesha bodaboda wa manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Nae Katibu wa waendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro Rashidi Omari, amesema ujenzi wa kituo hicho umekuja baada ya umoja wa waendesha bodaboda, kuomba serikali iwajengee, na kwamba kitasaidia kuwawezesha kutambuana hali itakayoepusha vitendo vya wizi kupitia mwavuli wa waendesha bodaboda.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga, amesema serikali ya mkoa wa Kilimanjaro imetenga maeneo ya kujenga vituo 100, na kwamba anawaomba wadau wa maendeleo kuchangia ujenzi wa vituo hivyo ili kuwapatia waendeasha bodaboda ajira endelevu.
No comments:
Post a Comment