Baadhi ya Wajasiriamali wakiwa katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye kongamano la wajasiriamali lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden mapema mwaka huu. Kongamano la namna hiyo linatarajiwa kufanyika Septemba 26, 2015 jijini Mwanza Ukumbi wa Benki Kuu (BoT), Capripoint.
Na Dotto Mwaibale
WAJASIRIAMALI zaidi
ya 250 wanatarajia kuonyesha bidhaa zao mbalimbali katika kongamano la mafunzo
ya ujasiriamali litakalofanyika jijini Mwanza.
Akizungumza na Dar es Salaam leo, Mratibu wa
kongamano hilo, Getrude Kilyabusebu alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa
mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wajasiriamali hao.
"Wajasiriamali hao katika kongamano hilo watapata fursa
ya kuonesha bidhaa zao mbalimbali na pia watapata mafunzo ya jinsi ya kukuza
mitaji yao na mbinu zingine za biashara" alisema Kilyabusebu.
Alisema makongamano ya namna hiyo yamekuwa yakiwasaidia
wajasiriamali hao kujuana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na utengeneza
wa bidhaa zao zikiwemo mbinu za ufugaji na kilimo.
Alisema mafunzo hayo utolewa na wataalamu waliobobea katika
shughuli za ujasiriamali na matunda ya mafunzo ya makongamano hayo yamewanufaisha
wajasiriamali wengi wajasiriamali.
Kilyabusebu alisema kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania
(Tanzania Business Entrepreneurs Women) lita Septemba 6, 2015 jijini
Mwanza katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT)
Capripoint.
Mratibu huyo alisema kuwa pamoja na mambo mengine kila
mshiriki atalazimika kuchangia gharama kidogo ili kufanikisha kongamano hilo
ambapo katika mafunzo na chakula atatakiwa kulipia sh.30,000, meza ya kuuzia
bidhaa na kuzitangaza sh. 20,000 na mafunzo na meza sh.50,000.
Kilyabusebu alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali wa
kanda ya ziwa kuweza kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kujifunza
stadi za kazi zao.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba 0754032589 /0756334078/0673032589
|
No comments:
Post a Comment