Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, November 25, 2015

PANONE FC YAMNG’OA MINZIRO


Timu ya Mpira wa Miguu ya Mkoa wa Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ikiwa inashikilia nafasi ya tatu katika kundi C huku kundi hilo likiongozwa na JKT Oljoro. Katika kuimarisha timu nakuongeza nguvu timu hiyo imekuwa moja ya timu ambazo zimeshtua wapenzi wa soka Tanzania kwa kuweza kuanza usajili na eneo muhimu katika timu huku wakihusisha mtu muhimu maarufu na mwenye mchango mkubwa katika soka la Tanzania.

Mwenyekiti wa bodi ya Panone Alhajj Mohamed Karia akifafanua jambo kwa Minziro


Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Panone Fc Alhaji Mohamed Karia Mara baada ya kuinyaka sahihi ya Aliyekua kocha wa JKT Ruvu Kocha Fred Felix Minziro kutoka Dar es salaam. Akizungumza kwa furaha Alhajj Karia alisema ilikuwa ni kazi ngumu kwao kuinyaka sahihi ya Kocha huyo kwa kuwa ni kocha mkubwa na ametoka katika klabu ambazo zipo daraja la juu na huku wakiwa na presha ya kumkosa kocha huyo kwa kuwa alikua akinyatiwa na club ya African sports ya Jijini Tanga lakini tayari sasa ni kocha wetu kwa kipindi cha mwaka mmoja. 


Alhajj Karia akipeana mkono na Minziro baada ya kumaliza kuweka sahhi mkataba.


“Ilitulazimu kumchukua na kukaa nae hotelini kwa muda wa siku tano huku tukifanyanae mazungumzo pamoja nakumpa wasaa wakuifahamu timu.Tunashukuru ameweza kuikubali timu na kuridhika kuweza kuwavusha wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwapatia timu ya ligi kuu” Alisema Alhajj Karia.

 Pia Mwenyekiti huyo wa bodi alitumia wasaa huu kuwaomba wakazi wa mkoa Kilimanjaro kuiunga mkono timu ya Panone kwanini timu ya Mkoa wa  Kilimanjaro na wasitoe mwanya wa maneno ambayo yanaweza kukwamisha ndoto za wengi.  

 

“Sina mengi ya kuongea nimeshukuru kwa uongozi wa Panone kwa kuweza kuniamini na sasa naomba wapenzi wa mpira na walimu wenzangu wa mpira tushiriki kuijenga timu ya panone fc” Alisema Minziro. Hata hivyo alipoulizwa kuhusu usajili Minziro alisema anategemea kuanza mechi za majaribio siku ya jumatatu nawachezaji takribani kuminasita kutoka sehemu mbalimbali wataungana na wachezaji waliopo wa Panone na kufanya mazoezi na mwisho ataweza kujua ni kikosi gani kitaweza kuingia kambini rasmi kwa ajili ya mazoezi na kujiandaa na Ligi inayotarajiwa kuanza mapema disemba 26.

No comments:

Post a Comment