Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 28, 2016

ALIYESHIKA NAFASI YA KWANZA KATIKA MTIHANI NCHINI INDIA AFUNGWA JELA

           Bi. Ruby Rai akiwa mikononi mwa polisi.

Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.

Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi.

Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.

Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.

Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.

                 Udanganyifu katika mtihani India


Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment