Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 15, 2016

SIMU FEKI KUZIMWA RASMI TAREHE 16/06/2016 - TCRA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSWnima_RcoXyPJwXnglbl-aQatBuQLmMLQYSJdRM2qlMOr1oG40kJBYGV22Rsc0u-C1rkArhvDr7IPgQVoOFS_a7Ul5dmTMkfLj-Wpg6CCPLOadYwPKKlpsbWpa8ALK5xFcFbj4lmAXqq/s1600/DSC_0299.JPG
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuzima simu feki ifikapo kesho Juni 16 mwaka huu.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjplo0IzFdq1NXF3IpBgCH8uwN2H9OGyBq9iyPF8y80q39Yud6Thmb_CBl5pBP8ubYndPVBSVHkE4HbX08GzGRi965YJF4EKhmHsvj35px5AYdUvZRsC52s6LUZekWshRXXUc4mSzvuo05N/s1600/DSC_0279.JPG
Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila kibuda, Globu ya Jamii.

SIMU ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi kesho, katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu kiwango kwa usalama  na ulinzi wa nchi.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.

Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa kutokana na kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10.

Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu wajiandae zoezi hilo na simu zitazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika mazingira salama.

Aidha amesema katika elimu wametoa hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.

‘’Simu feki kesho kuzimwa hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu simu ya  feki ambazo baada soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba.

No comments:

Post a Comment