Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 17, 2016

TAZAMA VIDEO YA RAY C AKIKAMATWA NA POLISI MAENEO YA KINONDONI

                                    Ray C


Kwa mujibu wa Mashuhuda ambao walikuwa eneo la tukio KINONDONI kama inavyoelezwa kwamba alifika eneo hilo ambapo kuna sehemu ya kuuza chakula (chips) na kusema "Mimi Ray C nataka kuvua nguo" mara akasema "Nishikeni kuna watu wanataka kuniteka" Ndipo ilipotokea Diffender (Gari ya Polisi) na kumbeba.

Esha Buheti ambae alikuwa eneo la tukio na kushuhudia yote aliandika haya kwenye Account yake ya Instagram

"Nashindwa hata niongee nini jamani, rayc Leo kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie rayc, I mean it jamani siku zote nlikua najua anaonewa ila nlichokishuhudia leoo nimeumiaa kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje? Nlikua na @kabulaflavour kino kwa wapemba tumefata chips mara tukaskia mtu anasema me rayc nataka kuvua nguoo, nikajua utani kushuka ni rayc anasema nishikenj kuna watu wanataka kuniteka, alikua na nguvu sana watu kamshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaaanza kugaragara kwenye matope akipiga KELELE kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari YA polisi ikambeba ila kwa tabu sanaa alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpk rayc anaondoka na ile gari yapolisi sikujua anapelekwa wapi alikua kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?"

No comments:

Post a Comment