Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, February 13, 2017

ALICHOKIZUNGUMZA T.I.D KWENYE MKUTANO WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

                                      T.I.D Msanii wa Bongo flava.

Mh. Mkuu wa Mkoa
Mh. Commissioner Siro
Ndugu waandishi, assalam aleykum!
Naomba kujitambulisha naitwa Khalid Mohamed na ni nimekuwa muathirika wa madawa ya kulevya.
Leo hii siko hapa kutoa historia kwanini, ilikuwaje nikaingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya hayo naomba tuweke kwa siku nyingine.

Nimekuja mbele yenu hapa kama kijana aliyepotea njia hapo nyuma na kuingia katika janga hili la taifa, kutoka moyoni mbele yenu nyinyi waandishi, Mh RC na wote wanaotazama na kusikiliza huko manyumbani kukiri nilikosea sana familia, mama yangu marafiki na jamii kwa ujumla na pia kuchukua fursa hii kuwaomba msamaha wale wote niliowakwaza when I was under drug influence. I pray that you all forgive me.

Nimesimama hapa kama kijana shupavu, mpambanaji, mwenye nguvu mpya lakini pia niko hapa mbele yenu kama "Mnyama" na niko tayari kuunga mkono vita hii ya madawa ya kulevya narudia tena "Mnyama" manake vita hii inabidi uwe mnyamaaa kama kakangu Makonda ili kuishinda.


Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kakangu Mh Makonda, najua wengi wanajiuliza imekuwaje kwanini? Lakini hakuna anayejua nimepitia mangapi mpaka kufikia hapa, labda nilihitaji nguvu ya dolla itumike ili nione uzito na ukubwa wa hili jambo.

Nakushukuru wewe binafsi Kakangu Makonda, Mh Raisi kwa kutuamsha sisi vijana na kuona kwamba hata serikali iko tayari kutusaidia kutokomeza shetani huyu, this is a wake up call for me sitorudi nyuma kamwe.

Natangaza rasmi kujiunga katika vita hii naomba M/Mungu atuongoze tuokoe maisha ya vijana wenzangu huko mitaani.
Naamini Muziki bila madawa inawezekana!!
Asanteni sana.

No comments:

Post a Comment