Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, March 9, 2017

Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa kufungua mkutano wa LAPF, kesho jijini Arusha

                


MFUKO wahifadhi ya wafanyakazi wa serikali za mitaa, LAPF,umeipongeza serikali kwakulipa malimbikizo ya madeni ambayo mfuko huo na mingine ilikuwa ikiidai kwamiaka mingi na hivyo kuathiri usitawi wa mifuko hiyo.

Meneja wa LAPFkanda ya kaskazini, Rajabu Kinande, amesema hatua ya serikali kulipa madenihayo kumeiongezea mifuko ya hifadhi ya jamii uwezo wa kuhudumia wanachama waokwa wakati. Kinande, ameyasemahayo Marchi 7 jijini Arusha, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa, AICC, kuelezea hatua ya maandalizi ya mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa wadau waLAPF.

Amesema mkutanohuo utafunguliwa na Waziri mkuu waJamhuri ya muungano wa Tanzania,Mh,Majaliwa KassimMajaliwa,Marchi 10 mwaka huu ambapo zaidi ya wanachama 1000 wa mfuko huo wanatarajiwa kuhudhuria.

Awali MenejaMawasiliano na Masoko wa LAPF,James Mloe, amesema kuwa kwenye mkutano huo kutawasilishwa mada mbalimbali zikiwemo Uendeshaji wa shughuli za mfukohuo,Hesabu zilizokaguliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)za mwaka 2015/16 ambapo mfuko huo umepata hati safi ya ukaguzi wa hesabu, ukusanyaji wa michango ulipaji wa mafao kwa wanachama na uwekezaji,Utawala bora na usimamizi wa uendeshajiwa mfukohuo na Raslimali fedha .

Amesema sikuya kwanza ya mkutano huo Marchi 9 kwa kuzingatia kuwa ni siku ya Figo dunianimfuko umeandaa upimaji wa figo bure kwa wanachama wote ambao utafanywa na Madaktari bingwa.

Mloe, amesema siku ya pili ya mkutano huo Waziri mkuu Kassim Majaliwa atazindua program mpya ya mikopo kwa wanachama kwa kushirikiana na benki ya CRDB, iitwayo Maisha popote ambao ni mkopo wa kwanza kutolewa na mfuko huo.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni kuibua fursa endelevu za ajira kwa maendeleo endelevu kwa watanzania. Kuhusu uwekezaji kwenye viwanda, Mloe amesema kuwa LAPF imeweka mitaji kwenye viwanda ambako tayari wameweka hisa zao.

Amesema kuwa LAPF haiwezi kujenga viwanda na kuvisimamia uendeshaji wake bali itaweka mitaji na kusisitiza kuwa LAPF itabakia kwenye jukumu lake la msingi la kulindamichango ya wanachama wake.


Na Pamela Mollel Arusha. 

No comments:

Post a Comment