Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, March 18, 2018

MGANGA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AFUNGA KAMBI YA WATOTO NA VIJANA YA AGPAHI MJINI MOSHI

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Magoma ambaye ndie alikua mgeni rasmi katika hafla ya kufunga kambi ARIEL CAMP 2018, akiingia huku akiwa ameambatana na watoto, vijana, wafanyakazi wa AGPAHI pamoja na wauguzi waliokua wakiwaangalia watoto na vijana wakati wakiwa kambini.

Mmoja kati ya watoto waliohudhuria katika ARIEL CAMP 2018 akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.

Mwakilishi wa wahudumu wa afya walioambatana na watoto, Bwana Aron Chasamawe kutoka Hospitali ya Wilaya ya Geita akizungumza kwa niaba ya wahudumu wengine.


Meneja Mawasiliano wa Shirika la AGPAHI, Bi Jane Shuma akizungumza kwa ufupi lengo la ARIEL CAMP 2018.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Magoma akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya watoto na vijana katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi hiyo inayopewa jina la ARIEL CAMP 2018.
 
Hawa ni watoto walioweza kuigiza kama familia inayoishi vizuri kwa kula mlo kamili na pia kula kwa wakati sahihi.

 Hawa ni watoto walioweza kuigiza kama familia inayoishi maisha duni, ambapo baba wa hii familia alionekana kuendekeza pombe kuliko kuijali familia.


Miss ARIEL CAMP 2018 akipewa mkono wa pongezi na mgeni rasmi Dr. Magoma.

Watoto waliopata nafasi ya kuwawakilisha wenzao katika tendo la kukata cake wakiwa na mgeni rasmi.

 
Mgeni rasmi alipata nafasi ya kuwakabidhi zawadi za mabegi zilizokua zimeandaliwa na shirika la AGPAHI, kwaajili ya watoto na vijana wote waliohudhuria kwenye ARIEL CAMP 2018.



  Mgeni rasmi pia aliwatunuku vyeti wahudumu wote wa afya waliokua wameambatana na watoto katika   kufanikisha kambi hiyo.





Meneja Mawasiliano wa Shirika la AGPAHI, Bi Jane Shuma akimkabidhi mgeni rasmi zawadi.

      
       Jumatatu ya Tarehe 12/13/2017 Shirika lisilo la Kiserikali la Arial Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)   lilianza kambi maalumu ya watoto na vijana wa Mikoa mitatu ya Tanzania kati ya Mikoa sita inayofanya kazi na shirika la AGPAHI. Leo ikiwa imetimia siku ya tano tokea mafunzo hayo ya kambi ya watoto yaanze.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Best Richard Magoma alifunga mafunzo hayo ya watoto na vijana katika hafla fupi ya ufungaji wa kambi hiyo inayojulikana kama ARIEL CAMP 2018 huku ikiwa na kauli mbiu “KIJANA EPUKA TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU.”

Meneja Mawasiliano wa Shirika la AGPAHI, Bi Jane Shuma aliweza kuzungumza kwa ufupi lengo la kambi kwa ambalo ni kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto na vijana. Washiriki wakiwa kambini hupata mafunzo ya afya pamoja na kushiriki kwenye michezo mbalimbali. Aliweza kutoa shukrani za dhati kwa walezi walioambatana na watoto, daktari bingwa wa watoto, mtaalamu wa saikolojia, muelimishaji rika na wafanyakazi wa Shirika hilo kwa ushirikiano wao walioonesha katika kipindi chote cha kambi.

Mbali na mafunzo ya darasani, Meneja Mawasiliano aliweza kuzungumzia juu ya matembezi yalifanyika kwa washiriki wa Kambi kutembelea  Kiwanda cha Soda cha Bonite Bottlers ltd, na kutembelea Kijiji cha Uru Msuni, kilichopo katika kata ya Uru Kaskazini wilaya ya Moshi vijijini na kujifunza mila na tamaduni za wachaga, kilimo cha kahawa na migomba.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Magoma, katika hotuba yake aliweza kutoa pongezi kwa shirika la AGPAHI kwa kuchagua Mkoa wa Kilimanjaro kufanyia mafunzo hayo huku akiwapongeza watoto na vijana kwa kuweza kujifunza na kuonesha kwa vitendo kile walichojifunza kwa siku zote hizo.

“Nimefarijika sana kuona mkiwa na tumaini kuu, hakika niwapongeze walezi wenu waliokua nanyi kwa siku zote hapa na kuwafundisha vyema, Nimetazama igizo lenu, limeelezea kile mlichojifunza na kudhihirisha kuwa mmeelewa. Sasa mkawe mabalozi wazuri kwa wenzenu maana nimepewa taarifa kuwa mpo zaidi ya watoto elfu tano (5,000) kwenye klabu mnazotokea na ninyi ni wawakilishi wa kundi hilo kubwa.” Alisema Dr. Magoma.

Kwa upande mwingine, mwakilishi wa wahudumu wa afya walioambatana na watoto, Bwana Aron Chasamawe kutoka Hospitali ya Wilaya ya Geita aliweza kuzungumza kwa niaba ya wahudumu wengine na kutoa pongezi za dhati kwa watoto kwa kuweza kuwa wasikivu na kuonesha nia ya kujifunza na wamepokea kile ambacho walitarajia kuwapatia katika Mafunzo. Pia hakusita kuonesha shukrani zake za dhati kwa shirika la AGPAHI kwa kuweza kuchagua watoto na vijana kama kundi muhimu katika vita dhidi ya Virusi Vya Ukimwi.
“Ni jukumu letu kuwasaidia vijana hawa, Ni vijana wenye hari, moyo wa kujituma na ndoto za kufika mbali na nina hakika watafika mbali” Alimaliza kwa kusema Bwana Chesamawe.

Dr. Magoma alimaliza ufungaji wa kambi hiyo kwa kuweza kuwapatia watoto na vijana zawadi ambazo ziliandaliwa na Shirika la AGPAHI pamoja na kuwatunuku vyeti wahudumu wote wa afya waliombatana na watoto na kufanikisha kambi hiyo.

Kilimanjaro Media iliweza kuzungumza na mmoja wa watoto hao baada ya kukamilika kwa kambi hiyo ambaye aliweza kuelezea furaha yake kwa kuweza kuwa mmoja wa watoto ambao wamewakilisha kundi kubwa la watoto  wenzao.
“Mimi nimetoka Tanga nimekuja katika kambi, lakini nilivyotoka Tanga na ninavyorudi ni tofauti, nimejivunza mambo mengi sana katika kambi hii.

No comments:

Post a Comment