Kufungua Kikao Kazi cha Maafisa Sheria na Rasilimali watu, kuzungumza na watumishi na kukagua Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Jumanne amewasili Jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo katika ziara hiyo amefungua Kikao Kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu, kuzungumza na Watumishi wa Umma pamoja na kukagua utekelezaji wa maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tanga.
Mhe. Waziri Kikwete akiwa mkoani Tanga amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian na kupokea mbalimbali za masuala ya utumishi na utawala bora.


No comments:
Post a Comment