Tanzania imesaini mkataba wa uenyeji wa mikutano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, Itifaki ya Kyoto na makubaliano ya Paris (UNFCCC) itakayokuwa ikifanyika Barani Afrika.
Tukio hilo ambalo ni la kihistoria, limeifanya Tanzania kuwa nchi pekee kusini mwa jangwa la Sahara kupata fursa hiyo ambayo itawezesha kuwa kinara wa jitihada za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akisaini mkataba huo Novemba 16, 2026, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema kufuatia kusainiwa kwa Mkataba huo Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mikutano miwili ya UNFCCC inayotarajia kufanyika februari 2027.

No comments:
Post a Comment