Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, October 12, 2026

π—£π—’π—Ÿπ—œπ—¦π—œ π—’π—‘π—šπ—˜π—­π—˜π—‘π—œ π—‘π—šπ—¨π—©π—¨ π—žπ—¨π—­π—¨π—œπ—” π—”π—π—”π—Ÿπ—œ - MHE. π—žπ—”π—§π—”π— π—•π—œ

 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kuongeza nguvu katika kukabiliana na makosa ya usalama barabarani kwa lengo la kuzuia vifo na majeruhi vinavyotokana na ajali za barabarani.

Mhe. Katambi ametoa agizo hilo, Oktoba 10, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa sheria za usalama barabarani ili kulinda maisha ya wananchi.

Pia, ameitaka jamii kusimamia maadili na kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, akieleza kuwa, malezi yenye misingi imara ya maadili ni muhimu katika kujenga taifa bora la baadaye.

Aidha, amezitaka mamlaka nyingine zinazohusika na ulinzi na usalama, ikiwemo Idara ya Uhamiaji, kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

Saturday, October 10, 2026

Australia’s Milton Dick succeeds Tanzania’s Tulia Ackson as IPU President





By TBN Reporter

ARUSHA, Tanzania, 9 October 2026 — Dr Tulia Ackson of Tanzania, who became President of the Inter-Parliamentary Union (IPU) after succeeding Portugal’s Duarte Pacheco in Luanda, Angola, in October 2023, has completed her three-year term, and was succeeded on Friday by Australia’s Speaker of the House of Representatives, Milton Dick, elected during the IPU’s 153rd Assembly in Arusha. 

Dick won 56 per cent of the vote in a single round of secret-ballot voting. Sahiba Gafarova, Speaker of Azerbaijan’s Milli Majlis, received 38 per cent, while Chilean Senator Rojo Edwards Silva received six per cent. Dick is the 32nd President of the IPU. 

Ackson was elected the IPU’s 31st President on 27 October 2023, at the 147th Assembly in Luanda. She was the first African woman to hold the office. 

Her successor, Dick, has represented the federal electorate of Oxley, Queensland, since 2016. He became Speaker of Australia’s House of Representatives in 2022 and was re-elected unopposed in 2025. 

After the result was announced, Dick called for unity among the organisation’s member parliaments.

“Today, there are no winners or losers. The IPU has spoken with one voice. This is democracy,” he said. “Dialogue still matters, respect still matters, cooperation still matters. We will work together, listen to one another and seek common ground.” 

As President, Dick will chair the IPU’s statutory meetings and represent the organisation at international events. He will work alongside IPU Secretary-General Anda Filip. 

The election marks a change in leadership for the global parliamentary organisation, as its members continue to address questions of democratic representation, international cooperation and the role of parliaments in responding to shared global challenges.



Friday, October 9, 2026

WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Arusha, Oktoba 8, 2026 

Wabunge kutoka Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Bara la Afrika kupitia Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU) wameunga mkono ajenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha afya ya uzazi, mama, mtoto na vijana barani Afrika.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha katika mkutano wa pembezoni wa Mkutano wa 153 wa IPU, ambapo viongozi hao pamoja na wadau wa maendeleo ya Sekya ya Afya Duniani wamejadili umuhimu wa kuimarisha sera, mifumo ya utoaji huduma, uwekezaji na uwajibikaji katika sekta ya afya.

Kiongozi wa Kundi la Kijiografia-Kisiasa la Wabunge wa Bara la Afrika kupitia IPU na Spika wa Jamhuri ya Chad Mhe. Ali Kolotou TchaΓ―mi, amesema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuunganisha nguvu, kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuwa na agenda ya pamoja ya kuboresha afya ya mama na mtoto.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Mhe. Angela Didiza, amesema Afrika inaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Tanzania katika kuendeleza afya ya wanawake, watoto wachanga, watoto na vijana, akisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa una nafasi muhimu katika kuweka mazingira ya utekelezaji wa hatua za kibunge.

Spika wa Bunge la Botswana, Mhe. Dithapelo Keorapetse, amesisitiza umuhimu wa kuunganisha uwekezaji katika sekta ya afya na ufuatiliaji wa matumizi na matokeo yake.

“Uwekezaji pekee hautoshi, bado tunakabiliwa na changamoto katika matokeo ya afya, hali hii inaonesha umuhimu wa kuangalia ufanisi wa matumizi ya rasilimali” amefafanua Mhe. Keorapetse.

Akizungumza, Rais wa Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema juhudi za Rais Samia katika kuimarisha afya ya uzazi zinapaswa kuungwa mkono, huku akisisitiza kuwa bila utashi wa kisiasa na uwajibikaji wa viongozi, wataalamu wa afya na na mifumo ya afya haitoshi kuimarisha Huduma za Afya ya uzazi, mama na mtoto. 

“IPU inajidhatiti kuwa mshirika wa vitendo kwa mabunge katika kuhakikisha ahadi zinatafsiriwa kuwa hatua na matokeo chanya ya kuimarisha Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto” amesema Dkt. Tulia.

Naye Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, amesema afya ya mama na mtoto ni kipaumbele cha Serikali ya Tanzania na kwamba Bunge kwa niaba ya wananchi lina wajibu wa kusimamia rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya huduma hizo.

Awali, Mshauri wa Rais kuhusu Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Mhe. Ummy Mwalimu, amesema vifo vitokanavyo na uzazi barani Afrika vimepungua kwa asilimia 42 kati ya mwaka 2000 na 2023, lakini Afrika bado inachangia asilimia 70 ya vifo vya kina mama duniani.

Amesema kupitia Mpango Kazi wa Rais Samia wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Barani Afrika 2026–2030, ajenda ya Rais Samia inalenga kufikia Sifuri Tatu: sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, na sifuri ya watoto wasiochanjwa.

SPIKA ZUNGU: TANZANIA IPO TAYARI KUCHANGIA UZOEFU HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO


Na Ripota wa TBN, Arusha.

Sika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Tanzania ipo tayari kuchangia uzoefu wake katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe na ustawi wa vijana.

Mheshimiwa Zungu ameeleza hayo Oktoba 8, 2026, wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika mdahalo kuhusu masuala ya afya ya mama na mtoto uliondaliwa na Serikali ya Tanzania wa wajumbe wa Mkutano wa 153 Umoja wa Mabunge Duniani. 

Mkutano huo unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Mheshimiwa Spika amesema afya na ustawi wa wanawake, watoto na vijana ni msingi wa maendeleo ya Taifa na kwamba Tanzania inatarajia kuchangia uzoefu wake na kufanya kazi na washirika kugeuza dhamira ya kisiasa kuwa matokeo ya kudumu.

“Kila kifo kinachozuilika, kila hitaji la kiafya lisilotimizwa na kila kikwazo cha kupata huduma,kinahitaji umakini na hatua endelevu za kisiasa.

“Ndio maana Rais wangu Mhe. Rais Hassan ameweka kipaumbele cha kupunguza vifo vya wajawazito, kupunguza vifo vya watoto na idadi ya watoto wasiochanjwa hadi sifuri, si tu nchini Tanzania bali pia kuchochea hatua hizi kote barani Afrika kupitia wadhifa wake kama Kinara wa Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika,” amesema.

Amesema Bunge lina jukumu la kuendeleza sheria, kuhakikisha fedha za kutosha  zinatengwa na kusimamia utekelezaji kuhakikisha rasilimali zinafika kwenye huduma za mstari wa mbele na kwa jamii.

“Kipaumbele chetu kiwe kwenye upatikanaji sawa wa huduma, ikiwemo huduma za mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe, na afya na ustawi wa vijana.

“Kupitia Mtandao huu, tunaweza kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kuimarisha uwajibikaji wa kibunge na kuendeleza hatua za vitendo katika nchi zetu. 

Kwa upande wake Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya afya, ustawi wa jamii, wanawake na watoto, Ummy Mwalimu aliyemuwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema Afrika imepiga hatua katika kupunguza vifo vya kina mama japo bado haijatosha.

Amesema vifo vya kina mama katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika vilipungua kwa asilimia 42 kati ya mwaka 2000 na 2023, lakini Afrika bado inachangia takribani asilimia 70 ya vifo vya kina mama duniani.

“Kwa kasi iliyopo sasa Afrika haitaweza kufikia lengo la Maendeleo Endelevu la kuwa na vifo vya kina mama 70 kwa kila vizazi hai 100,000 hadi karibu mwaka 2050,” amesema Mwalimu.

Mwenyekiti wa Kundi la Kijiografia la Afrika la IPU, Mhe. Ali Kolotou TchaΓ―mi amesema Wabunge wana wajibu wa kuhakikisha ahadi za afya zinawafikia wananchi wa kawaida.

Amesema watunga sheria wana jukumu la kutunga sheria, kuidhinisha bajeti na kusimamia serikali, hususan katika kulinda makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.

Akitoa mchango wake katika mkutano huo, Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Angela Thokozile Didiza, ametoa wito wa kuimarishwa kwa uongozi wa kisiasa, akibainisha kuwa vifo vya kina mama na chanjo za watoto bado ni changamoto kubwa za afya ya umma.

IPU Chief Praises Tanzania’s Progress on Women’s Political Representation

 


By TBN Reporter, Arusha

Inter-Parliamentary Union (IPU) Secretary-General Anda Filip has praised Tanzania’s progress in increasing women’s representation in politics and leadership, saying the country’s experience could offer useful lessons to other nations seeking more inclusive decision-making.

In a special interview in Arusha on 7 October, during the 153rd IPU Assembly, Filip said she was encouraged by the growing representation of women in Tanzania’s Parliament, which she put at more than 39 per cent.

She stressed that women must have meaningful opportunities to participate in political processes and national decision-making. Filip also said Tanzania’s Development Vision 2050 offered an opportunity to strengthen the involvement of women and young people in shaping and carrying out the country’s long-term development agenda.

Tanzania is represented at the Arusha Assembly by eight members of Parliament. Five are women, making up 62.5 per cent of the delegation, while three are men, or 37.5 per cent.

The women delegates are Dr Pindi Chana, Dr Zeyana Hamid, Kiza Myeye, Engineer Fatma Rembo and Asha Feruzi. The men are Dr Damas Ndumbaro, Elibariki Kingu and Rashid Shangazi.

The 153rd IPU Assembly opened at the Arusha International Conference Centre on 5 October and is scheduled to conclude on Friday, 9 October. The gathering brings together parliamentarians from around the world to discuss parliamentary action on inclusive governance and other global issues. 

Filip took office as IPU Secretary-General on 1 July 2026, becoming the first woman to hold the post in the organisation’s history.

Thursday, October 8, 2026

WAZIRI ULEGA AANZA VIKAO NA IDARA ZA WIZARA

 


Ikiwa imepita siku moja mara baada ya  kukutana na Menejimenti ya Wizara, Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Abdallah Hamis Ulega, leo  Oktoba 8 , 2026  ameanza ratiba ya kukutana na Idara za Wizara kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji wa kazi pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali.

Hatua hiyo  ni sehemu ya utaratibu wa Waziri Ulega kujenga uelewa wa kina kuhusu majukumu na utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Katiba na Sheria, kufuatia kuhamishiwa Wizara hiyo kutoka Wizara ya Ujenzi.

Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki imewasilisha majukumu na shughuli zinazotekelezwa katika Idara hiyo.

Waziri Ulega pia atakutana na Idara na Vitengo vya Kisheria ikiwemo  Idara ya  Huduma za Msaada wa Kisheria, Haki za Binadamu, Idara ya Huduma za  Huduma za Kisheria kwa Umma, Kitengo cha Uangalizi wa Utajiri  wa Asili na Maliasilia za Nchi pamoja na Kitengo cha Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala.

Kikao hicho  kimehudhuriwa na Naibu Waziri, Mhe. Zainab Athuman Katimba; Katibu Mkuu, Dkt. Seif Shekalaghe; na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Baraka Haran Luvanda.

IPU Yaisifu Tanzania Kwa Kuongeza Uwakilishi Wanawake Bungeni

 




Na Ripota wa TBN, Arusha. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Anda Filip, ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyopiga katika kuongeza idadi ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi, na kueleza kuwa uzoefu wa Tanzania unaweza kuwa somo kwa mataifa mengine katika kujenga mifumo jumuishi ya kufanya maamuzi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Oktoba 7, 2026 wakati wa Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika Arusha, Filip amesema anavutiwa na namna Tanzania ilivyoongeza idadi uwakilishi wa wanawake katika Bunge la Jamhurin ya Muungano wa Tanzania, ambao kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 39.

Katika mkutano huo, Mhe. Filip amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya kisiasa na maamuzi ya kitaifa.

Filip amesema kupitia Dira ya Maendeleo 2050, Tanzani ina fursa ya kuimarisha ushiriki wa wanawake na vijana katika kujenga na kutekeleza ajenda za maendeleo ya muda mrefu, ili kuhakikisha vipaumbele vya taifa vinaendelea kutekelezwa na vizazi vijavyo bila kutegemea mabadiliko ya awamu za uongozi.

Katika mkutano wa IPU unaendelea jijini Arusha, Tanzania inawakilishwa na Wabunge nane ambapo kati ya hao, Wabunge wanne ni wananwake ikiwa ni sawa na asilimia 62.5 ya uwakilishi wa wanawake wanaoiwakilisha Tanzania katika Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Wabunge hao wanawake ni Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana, Mheshimiwa Dkt. Zeyana Hamid, Mheshimiwa Kiza Myeye, Mheshimiwa Mhandisi Fatma Rembo na Mhehimiwa Asha Feruzi. 

Wabunge wengine waliopo IPU ambao ni wanaume ni Mheshimiwa. Dkt. Damas Ndumbaro, Mheshimiwa Elibariki Kingu na Mheshimiwa Rashid Shangazi, ambao idadi yao ni sawa na asilimia 37.2 ya uwakilishi wa wabunge wa Tanzania.

Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani ulianza tarehe 5 Oktoba, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) na unatarajia kuhitimishwa Ijumaa Oktoba 9, 2026. Mkutano huu umeshirikisha wajumbe zaidi ya 2000 kutoka mataifa mbalimbali.