ZIMEKATIKA siku 75 tangu kufariki dunia kwa supastaa wa filamu za Bongo, Steven Charles Kanumba, Aprili 7, 2012. Mama mzazi wa marehemu huyo, Flora Mtegoa mambo yamemnyookea ambapo amenunua jumba kubwa la kifahari, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kuripoti. CHANZO CHATEMA NYETI Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, mjengo huo upo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam ambapo mama huyo na familia yake (akiwemo Seth Bosco) wamehamia. Sanjari na wao, pia magari matatu ya marehemu, Toyota Hiace, Toyota Lexus na Toyota GX 110 yamepiga kambi huko, kila moja likiwa na sehemu yake ya kuegesha. Kwa mujibu wa chanzo hicho, kwa sasa mama Kanumba hana makazi tena pale Sinza Kijiweni ambako ndiko palipofanyikia msiba wa mwanaye hadi kuhitimisha na arobaini yake. Paparazi: Inasemekana mmehama pale Vatican, mmehamia wapi? Seth: Aaa, tumehamia Temboni huku. Paparazi: Ni kweli huko mmenunua nyumba? Seth: Ni kweli. Paparazi: Shilingi ngapi? Seth: Mh! Hilo swali anayeweza kujibu ni mama kwamba ni shilingi ngapi na mambo mengine yote. Risasi Jumamosi lilipomsaka mama Kanumba kwa kutumia simu yake ya mkononi, hakupatikana hewani siku hiyo. MJENGO WA BEI MBAYA Hata hivyo, Risasi Jumamosi lilifanya uchunguzi na kunyaka baadhi ya nyaraka zinazoonesha kuwa mjengo huo umenunuliwa kwa shilingi milioni themanini (80,000,000) za Kibongo. MASTAA HAWAJUI Gazeti hili lilijaribu kufanya mawasiliano na baadhi ya mastaa wa filamu Bongo kama wanajua mama yao huyo amehama Sinza lakini kila aliyeulizwa hakuwa anafahamu na kuwa ‘sapraizi’ kwake. Mwanyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Jacob Steve ‘JB’ alipovutiwa uzi na kuulizwa alisema hajui kama mama Kanumba amehama Sinza.
Banner
FOLLOW US FACEBOOK
propertyfinder.co.tz
Saturday, June 23, 2012
MAMA KANUMBA ANUNUA JUMBA LA KIFAHARI

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment