Na mpaka sasa tayari kuna baadhi ya wasanii ambao kupitia S.U.A project wamesha record nyimbo, pia kuna event kama mfano wa Project ya OKOA MTAA ambayo itazinduliwa mwisho wa huu mwaka.....Kwa maswali, msaada ama ushauri tuandikie kwenye suafreestage@gmail.com........
Juhudi zote hizo za kuibua vipaji zinafanyika na Members wa Watengwa records iliyopo kijenge juu, Na nilifanikiwa kuonge na "JCB" mmoja kati ya Artist wa watengwa records na akanijuza machache kuhusiana na mpango mzima wa S.U.A alifunguka kwa kusema hivi "Maana ya S.U.A ni Saving Underground Artists, na hii project tumeianzasha maususi kwa ajili ya ya kusaidia underground artists wenye vipaji lakini hawana uwezo wa kwenda studio kurekodi ngoma zao, na tamasha hilo linafanyika kila baada ya wiki mbili nje ya studio ya watengwa records na hakuna kiingilio kwa yeyote anayependa kushiriki katika tamasha hilo.. Tunawakaribisha watu wa rika zote kuja kushuhudia juhudi walizonazo vijana wa Arusha katika kujikwamua kimaisha kupitia muziki" hivyo ndivyo alivyomaliza "JCB" mmoja kati ya MC's ambao kwa mwaka jana aling'ara sana kwenye tuzo za kili music awards kwa kupata tuzo mbili na kuudhitishia uma kwamba Arusha ndio HIP POP City,,, baada ya hayo aliendelea na story na michakato mingine ya kitaa...
Mengi zaidi kuhusiana na S.U.A na Watengwa kwa ujumla utaendelea kuyapata hapa hapa ..
No comments:
Post a Comment