Waziri mkuu Mh. Peter Pinda
Serikali imesema bado kuna umuhimu mkubwa wa mbio za mwenge kwani licha yakuwa ni alama ya taifa lakini pia hutumika katika kuzindua miradi mbalimbali na kutukumbusha juu ya umoja, amani na mshikamano wetu.
Akijibu maswali ya papo kwa papo hii leo waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema kuwa mbio za mwenge zimekuwa njia ya kuwafikishia ujumbe wananchi kupitia kauli mbiu mbalimbali.
Kuhusu zana iliyo jengeka kuwa mbio za mwenge ni zinatoa nafasi kwa watu kujiingiza katika ngono zembe Mh.Waziri mkuu amesema swala la ngono zembe lipo sehemu mbalimbali hivyo niswala kila mmoja kichukua tahadhari binafsi.
Mwenge wa uhuru kwa mara ya kwanza uliwashwa tarehe 09 December mwaka 1961 nakupandishwa katika kilele cha mlima kilimanjaro na baada ya hapo ulihifadhiwa hadi mwaka 1964 ulipo washwa tena na kuanzakukimbizwa tena , ambapo mwaka huu uliwashwa mkoani mbeya ukiwa na waulimbiu ya kuhamasisha watu kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya taifa itakayofanyika nchi nzima Augost 26 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment