Jacqueline Wolper.
Na George KayalaIMANI ya Freemason inayodaiwa kumteka staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper imetiliwa shaka na Askofu Mark Diganyeka wa Kanisa la Good News for All Nations lililo chini ya Huduma ya Rock Ministry, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Motomoto Newz, Askofu Diganyeka alisema anaamini msanii huyo si muumini wa Freemason kama wengi wanavyodai kwa vile haoni kigezo cha yeye kuwa muumini wa imani hiyo.
“Sidhani kama Wolper ni mfuasi wa Freemanson kama inavyodaiwa, Watanzania waondokane na kasumba ya kuamini kila anayepata fedha kwa haraka ni Freemason.
“Suala la utajiri linatokana na juhudi za mtu katika kusaka mafanikio,” alisema askofu huyo ambaye naye aliwahi kuwa kwenye imani hiyo.
No comments:
Post a Comment