MSANII Naseeb Abdul ‘Diamond’,
ambaye ni mtoto wa dini ya Kiislamu,amesema kuwa anawatakiwa mfungo
mwema mashabiki wake wote wa dini hiyo ambao wanafunga mwenzi
huu mtukufu wa Ramadhani kwani anaamini kipindi hiki kitakuwa ni kuzuri
kwa ajili ya kutubu na kutafakali juu ya masuala mbalimbali.
Akiongea na DarTalk msanii
huyo alidai kuwa hawezi kushindwa kutoa maneno hayo ya kuwatakia mwezi
mtukufu mashabiki kwani ni watu ambao amekuwanao kwa kipindi kirefu na
wamempa sapoti kubwa katika kila kazi anayoitoa.
Alisema kuwa anaamini hata kwa upande kipindi hiki cha mwezi mkutukufu
anatakuwa akitafakali mambo mengi likiwemo muziki kwani bila mungu
hakuna anayeweza kufanikiwa.
“Naamini kipindi hiki watu hasa wale wa dini ya kiisilamu watakuwa
katika mfungo hivyo nawatakia mfungo mwema, katika kipindi chote
watakachokuwa katika ramadhani, pia nawakumbusha tu kwamba kutenda mema
si kipindi hiki pekee bali siku zote wanatakiwa kutenda mema,” alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment