John Mnyika: Sekta ya afya taifa linarudi nyuma kwa ari, nguvu na kasi zaidi; Tuungane kumshauri Rais...!
John Mnyika
Kwa
Sekta ya afya taifa linarudi nyuma kwa ari, nguvu na kasi zaidi;
tuungane kumshauri Rais kuingilia kati kuwezesha wigo wa mapato
kupanuliwa kupitia marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha na hatimaye
tuletewe bajeti ya nyongeza kwa ajili ya sekta ya afya tupunguze
upungufu wa madawa, vifaa tiba na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma
kwenye sekta ya afya wakiwemo madaktari. Bajeti iliyopitishwa leo
utegemezi wa fedha za nje kwenye fedha za maendeleo umeongezeka na
kufikia asilimia 93 kwa bajeti ya 2012/2013 wakati kwa mwaka 2011/2012
wahisani walitimiza ahadi zao kwa asilimia 36 tu pamoja na kuahidi zaidi
ya asilimia 90. Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013
imeshuka mpaka asilimia 10.4 tu ya bajeti ya Serikali wakati wastani kwa
miaka sita mfululizo nimepiga mahesabu ilikuwa ni asilimia 11. Serikali
imekiri bungeni kuwa kiwango cha bajeti kinachotengwa kwenye sekta ya
afya kinapungua badala ya kuongezeka kufikia asilimia 15 ambayo
iliridhiwa Abuja mwaka 2001 zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Kilichonisikitisha zaidi ni kuwa Waziri amesema kuwa Rais atahakikisha
lengo hilo linafikiwa ifikapo 2015. Tujadili kwenye bunge la wananchi na
kuchukua hatua, Maslahi ya Umma KWANZA
No comments:
Post a Comment