Kwa mara
ya
kwanza kifaa cha kujipima iwapo mtu ana virusi vinavyosababisha ukimwi
kimeidhinishwa na wataalam wanaodhibiti sekta ya Afya nchini
Marekani.
Kifaa hicho kwa jina OraQuick kitawezesha watu kutumia
mate kuchunguza kama wana virusi vya ukimwi.
Itachukua
muda
wa kati ya dakika 20 na 40 kubaini matokeo ya uchunguzi huo.
Kifaa hicho ambacho kitawezesha mtu
kuchunguza hali yake mwenyewe nyumbani au kokote anakotaka kitaanza
kuuzwa nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka huu.
Serikali ya Marekani inatarajia kuwa
kifaa hicho kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa
kubadili tabia miongoni mwa watu wanaoishi na virusi bila kujua.
Inakadiriwa kuwa robo millioni ya
Wamarekani wako katika kitengo hicho.
Utafiti wa kimatibabu unaoyesha kuwa
majaribio ya matokeo ya uchunguzi wa kifaa hicho cha Oraquick
yananaweza kuwa sahihi kwa asilimia tisini na mbili, miongoni mwa watu
wanoishi na virusi vya ukimwi.
No comments:
Post a Comment