Lema amvaa Ridhiwani Kikwete...!
Hii nimeitoa kwenye kwenye facebook page ya kamanda Lema wa Arusha.....
Naomba hili liwe wazi kwa Watanzania, Ridhiwan Jakaya Kikwete, chini ya
kampuni ambayo wanaharakati tutaleta ushahidi wake kwa wananchi
wanaotaka ukombozi, wiki hii alikuwepo Jijini Arusha na tayari ana
mkataba wa umiliki wa zaidi ya hisa asilimia 45 za kampuni ya Tanzanite
One. Hii ni biashara ya Rais wa nchi. Ametumia madaraka yake kwa siri
kupisha umiliki huu kupitia mtoto wake. Linaweza kukanushwa na kupingwa
lakini muda unafika ambapo umma wa Watanzania utaamua. Hata wakishinda
kesi za mahakamani, hawataushinda uamuzi wa umma. CCM inakufa, iko
hatua za mwisho kabisa.
No comments:
Post a Comment