Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
Mradi huo umezinduliwa leo na mke wa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania Mama
Tunu Pinda akiwa ndio mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambapo katika
kuuzindua mradi huo uliopata kuhudhuriwa na waandishi wa habari,maafisa
kutoka ngazi mbalimbali serikalini mkoani hapo na wananchi wa mkoa wa
Kilimanjaro, mama Pinda alielezea kufurahishwa kwake na juhudi zinatofanywa na kampuni ya bia ya Serengeti katika kuisadia jamii ya watanzania bila kupendelea upande wowote.
“Mimi
nashukuru sana kwamba leo nimepata fursa ya kusema yale niliyonayo
moyoni kwa mda mrefu, kwamba kampuni hii ya bia ya Serengeti kwakweli
mnafanya mambo makubwa ambayo hata serikali haikutegemea kama mtafanya,
mmekua mstari wa mbele sana katika kuisaidia jamii inyowazunguka
kwakujenga miradi mikubwa hasa yale yenye tija na na muhimu
katika maisha ya kila siku kwa watanzania” aliseam mama Pinda huku
akiwataka wakazi na watumiaji wa hospitali ya mawenzi mkoani Kilimanjaro
na watanzania kwa ujumla kujenga imani na mahusiano mazuri na makampuni binafsi hasa yanayojali wateja wake na wananchi kwa ujumla kama kampuni ya bia Serengeti.
“Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu kampuni hii hii yani Serengeti Breweries
ilipozindua mradi mkubwa sana wa maji huko mkoani Iringa na ndio maana
nawapongeza sana kwamba mnawajali na kuwasaidia watanzania bila kubagua,
najua kuwa mliwahi kujenga mradi mkubwa wa maji Mkuranga jiji Dar es
Salaam na kwa sababu
hiyo sasa ifike mahali jamii ya watanzania waamini na kutambua kuwa
kuwepo kwa kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchi kumeleta faida kubwa
kwa sereikali na kwa jamii hongereni sana Serengeti breweries kwa juhudi
zenu za dhati kabisa za kuinua uchumi ya watanzania” alisema mama
Pinda.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni ya bia ya
Serengeti Bi. Teddy Mapunda, amesema mradi huo uliogharimu zaidi ya
milioni 50 za kitanzania ulilenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yayoikumba
jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya
mtanzania, “sisi kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto
zinazowakabili watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama,
na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya Serengeti imeona hilo na kuamua
kusadia kutatua tatizo hilo katika maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa haraka zaidi”
alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii ni moja yab
sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha shukrani zake kwa
wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu
ya kampuni ya bia ya Afrika Mashariki iliyopo chini ya kampuni za
Diageo inayoongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa vinywaji vikali na
kufikia zaidi ya nchi 180 duniani,Serengeti Breweries ikizalisha Serengeti Premium Lager, Tusker Lager, Tusker Malt Lager, Senator, Pilsner, The Kick, Uhuru Peak Lager.
No comments:
Post a Comment