Vincent Kigosi ‘Ray’.
Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Na Erick Evarist, TangaMASTAA wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamewaacha wakazi wa jijini Tanga midomo wazi baada ya kuonesha umahiri mkubwa wa kuzungusha nyonga zao, Tollywood Newz ilishuhudia.
Mpango mzima ulijiri katika Viwanja vya Tangamano jijini hapa kulikokuwa na uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu (Tanzania Open Film Festival) ambapo ulifika wakati wa utambulisho wa msanii mmoja baada ya mwingine ndipo wasanii hao walipovunja rekodi ya kukata mauno baada ya kuwekewa muziki.
“Mh! Kweli nimeamini Ray alikuwa mcheza ngoma maana ameonesha ujuzi wa hali ya juu wa kukata mauno,” alisema Ally Baruhan mkazi wa Tanga.
No comments:
Post a Comment