|
“Bodi ya Wakurugenzi wa NBC imepokea malalamiko ya wafanyakazi kuhusu kuwapo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kiutendaji katika uongozi wa benki.” Alisema Assad katika taarifa hiyo na kuongeza: “NBC ni benki inayoheshimika na kuaminika, kwa hiyo ili ya kulinda taratibu na misingi ya utawala bora, imeanza kufanya uchunguzi wa kina na sahihi juu ya tuhuma hizo. Ili kufanijkisha kazi hiyo, Bodi ya Wakurugenzi imeamua kumpa likizo Mafuru ili kupisha uchunguzi huo kufanyika. Naamini kazi hiyo itakamilika mapema iwezekanavyo.” Naye mafuru kwa up-ande wake alisema; “ Nitatoa ushirikiano kwa dhati kuhakikisha kuwa uchunguzi juu ya tuhuma zinazonikabili unafanyika kwa uhuru na haki.” |
Bodi
ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC imemsimamisha kazi kwa kumpa likizo
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo , Lawrence Mafuru kupisha uchunguzi
wa kukiuka taratibu za utendaji ndani ya taasisi hiyo maarufu ya fedha
nchini.Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jana na benki hiyo na
kutiwa saini na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Mussa
Assad, uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia malalamiko ya wafanya wa NBC
yakimtuhumu Mkurugenzi huyo kuwa alikuwa anakiuka taratibu za
kiutendaji.
No comments:
Post a Comment