HILI NI ENEO LA STAND YA MOSHI AMBALO KWA KAWAIDA HUWA NA MAGARI
MENGI SANA LAKINI BAADA YA MAGARI KUGOMA HALI NDIO ILIVYO KWA SASA.
WANAUSALAMA NAO HAWAKUWA MBALI NA ENEO LA STAND ILI KUHAKIKISHA
RAIA NA MALI ZAO WAPO KWENYE HALI YA USALAMA MUDA WOTE.
HAWA NI BAADHI YA ABIRIA WAKIWA KATIKA HALI ZA MASIKITIKO
WAKISUBIRI HATIMA YA MGOMOWA MAGARI YA ABIRIA..
ABIRIA WENGINE WALIKUWA NA MIZIGO NA HAWAJUI WAELEKEE WAPI MAANA HALI ILIKUWA INAKATISHA TAMAA MAANA HAKUKUWA NA GARI HATA MOJA YA ABIRIA ENEO LA STAND YA MOSHI MJINI.
ABIRIA WAKIWA KWENYE MAKUNDI WAKIJADILI HATIMA YAO YA KUPATA USAFIRI.
WAKATI WOTE WA MGOMO WA MAGARI YA ABIRIA KWA UPANDE WATU WA BODABODA (PIKIPIKI) NA TAX KWAO ULIKUWA NI WAKATI WA MAFUNO, MAANA ABIRIA WALIOKUWA NA UWEZO ILIBIDI WAKODISHE PIKIPIKI AU TAX.
HAWA NI BAADHI YA MADEREVA NA MAKONDAKTA WALIKUWA KWENYE MGOMO,
WAKIWA WAMEKAA MAENEO YA STAND WAKIWATIMA MADEREVA WA PIKIPIKI NA TAX WANAVYOPAKIA ABIRIA.
No comments:
Post a Comment