Bodi
ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni
2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi
sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika
kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki
moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.
Baada
ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza
yafuatayo:(i) Madaktari waliopo kazini waendelee na
kazi kama kawaida;(ii) Madaktari waliogoma warejee
kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa
Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya
mwaka 2004.(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini
mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao
umeandaliwa. (iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua
za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na
kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na
taratibu za kazi;(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara
moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo
(interns); na(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange
(re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo
yaliyoathirika wakati huu wa mgomo
Aidha,
Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao
wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile,
Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira
na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya
taaluma zao.
_________________Dkt. Gabriel UpundaKAIMU MWENYEKITIBODI YA WADHAMINI
No comments:
Post a Comment