Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa.
Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi.
Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani.
Gazeti
moja la kila wiki limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa
madai kwamba ni habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.
Idara inataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni zaUZUSHI NA UONGO ambazo
zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa
zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali ili kukidhi
malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumiagazeti
hilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa
katika tuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.
Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.
Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja
moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azma yetu ya
kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na
wanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.
No comments:
Post a Comment