MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini
Jacqueline Massawe ambaye ni maarufu kwa jina la WOLPER amesisitiza kwamba
amebadili dini na kwa sasa anajiandaa kwa kuupokea na kufunga mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Akizungumza katika chombo kimoja cha
habari Luninga WOLPER amesisitiza kwamba yeye hivi sasa ni muislamu na
amejitayarisha kufunga na kujizuia kufanya shughuli za kisanii ambazo
zitamsababishia kutengua saum yake hivyo kwa kipindi hicho cha muda wa mwezi mmoja
atakuwa akijishughulisha na kazi zake zingine.
"Unajua dini ni imani na hii iko
ndani ya moyo wangu hivyo nachukizwa kwa kitendo cha baadhi ya ndugu zangu wa
karibu kuniita MALAYA na hukumu kwa mambo mbalimbali mimi ndiyo najua na fanya
nini katika maisha yangu"alisema.
Aidha amewatupia dongo wale wote wanao
mmtupia maneno ya kumdhihaki kwamba hatoweza kufunga na kuswali , "Unajua
tumepewa miezi 11 ambayo tuko huru kufanya mambo mbalimbali ya starehe za
kidunia kwanini nishindwe kujizuia ndani ya mwezi mmoja tu, mimi nasema
hivi nitasali sitakuwa na makucha , manywele na mambo mbalimbali
ambayo hayapendezi katika ibada".
No comments:
Post a Comment