Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kimotoroko Wilaya ya
Simanjiro
Mkoani Manyara wamefariki dunia baada ya nyumba yao
walimokuwemo
ndani kuungua na kuteketea kwa moto kabisa.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani
Kilimanjaro ,Akili
Mpwapwa wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani
manyara.
Aidha kamanda Mpwapwa amesema kuwa tukio hilo lilitokea hivi
karibuni
majira ya saa 10:00 jioni huko kimotoroko.
Amewataja watoto hao kuwa ni Luman Lck(5) na mdogo wake
wenye umri
wa miezi minane(8) Leman lack ambao waliungua ndani ya
nyumba yao na
kufariki dunia papo hapo.
Amebainisha kuwa chanzo cha moto huo ni kwamba watoto hao
waliachwa
nyumbani wakichochea moto uliokuwa ukichemsha maharagwe
jikoni huku
wazazi wao wakiwa wameenda kuchunga mifugo.
Ameongeza kuwa katika harakati za kuchochea moto ndipo moto
huo
uliposhika chupa iliyokuwa na lita moja ya mafuta ya petroli
iliyokuwa
karibu na moto huona kupelekea kulipuka na kushika nyumba
hali
iliyopelekea kuungua na kuteketea kabisa.
No comments:
Post a Comment