Kiongozi moja mkuu wa kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni mbunge mteule ameshtakiwa kwa kuchochea ghasia.
Mbunge Sheikh Mohammad Dor (pichani) alisema kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani.
Mbunge Sheikh Mohammad Dor alisema kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani.
Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo Omar Mwamnuadzi.
Sheikh Dor
alikamatwa jana jioni baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza
kufadhili vuguvugu hilo, ingawa aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana
ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka ya uchochezi.
Kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe kumi na tatu mwezi Novemba.
Sheikh Dor
ambaye amelaani msako unaoendelea wa polisi dhidi ya kundi hilo mjini
Mombasa, alisema kuwa kundi hilo ambalo mahakama ilisema kuwa sio
haramu, kwa mtu kuamua kulifadhili sio kosa.
Dor ni mmoja wa wabunge kumi na wawili wa Kenya ambao hawakuchaguliwa ingawa waliteuliwa kuwakilisha maswala kadhaa bungeni.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment