MAMLAKA ya Majisafi na taka Manispaa 
ya Musoma mkoani wa Mara (MUWASA) imewashusha waandishI wa habari njiani 
waliokuwa katika ziara ya Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Dk.Eng.Binilith 
Mahenge  kwa madai  ya kisingizio cha ufinyo wa 
bajeti.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa 
magezeti ya mbalimbali mkoani hapa wameshushwa katika eneo la ofisi ya Mkuu wa 
wilaya ya Manispaa ya Musoma na  Afisa Mahusiano wa 
 Mamlaka hiyo Emmanuel Ruyobya  hali ambayo ni 
imeonekana kuwa ni udhalilishaji.
 “Kiukweli huu ni udhalilishaji 
kwani sisi tuna vyombo vyetu ambavyo tunavifanyia kazi na si lazima tulipwe 
posho sasa huyu yeye anasema bajeti finyu wakati sisi hatujaomba posho” alisema 
mmoja wa waandishi wa 
 
habari walioshushwa katika gari hiyo.
Akisoma taarifa  ya 
Maendeleo na Changamoto zake katika ofisi ya mkuu wa mkoa kwa Naibu,Katibu 
Tawala wa mkoa hupo Climent Lujaji alimuagiza mkurugenzi wa MUWASA Genes Kaduri 
kuwaweza waandishi hao katika suala la usafiri ili waweze kushiriki katika ziara 
hiyo ambapo mkurugenzi huyo alimkubalia .
Aidha Baada ya kuondoka katika eneo 
la ofisi wa mkoa waandishi wa habari hao walishishwa katika gari hiyo kwa madai 
hayo na kwamba wameishaalika waandishi wao .
“Kama 
Katibu Tawala wa mkoa  ndiye kawaambia muje  
nendeni  awalipe na kuwatafutia usafiri.,alisema Afisa 
mahusiano  Ruyobya kwa jaziba kubwa.
Tabia ya kuwashusha waandishi wa 
habari  si la mara ya kwanza katika ziara mbalimbali zinazofanywa 
na viongozi kama hao mkoani hapa hususani katika vyombo habari  vya 
magazeti kubaguliwa  na hata hivi karibuni 5 Oktoba mwaka 
huu  imefanyika ziara ya Naibu waziri wa Nishati na Madini Stephen 
Masele  ambapo pia vyombo vingine vimebaguliwa.
Naibu 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Binilith Mahenge 
 ameaza ziara yake ya kujua maendeleo na changamoto zake  
mkoa wa Mara  ambapo imeanzia katika halmashauri ya wilaya 
ya Manispaa ya Musoma,Butiama kukagua  chanzo cha maji cha Mugango 
–Kiabakari, Rorya,Serengeti na kumalizia wilaya ya Bunda.
 
 
 
No comments:
Post a Comment