WATU watatu, wakiwamo waandishi wawili, Hussein Semdoe wa gazeti la
Mwananchi na Hamis Bwanga wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo na Ofisa
Uhamiaji wa Wilaya ya Handeni, Mariam Hassan wamefariki papo hapo katika
ajali ya kutisha iliyotokea leo Misima, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Marehemu Hussein Semdoe akiwa kazini. Picha hii ilipigwa mwishoni mwa wiki Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga
Watu hao walikuwa wakitoka Misima katika shughuli za kikazi na
kusababisha vifo hivyo vilivyopokelewa kwa uchungu mkubwa na Watanzania
wote, wakiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Afisa Elimu Shule za Sekondari wilayani
humo, Simon Mdaki, alisema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari
walilokuwa wanasafiria kupasuka tairi, hivyo dereva kulishindwa na
kupinduka.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu
akiwa kwenye kazi za kijamii Kwedikabu, Kwamsisi mwishoni mwa mwaka jana. Mwenye Kamera ni marehemu Semdoe. |
Alisema ajali hiyo ilikuwa nyuma ya gari ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni,
Rweyemamu, aliyeambatana na watu hao ambao kwa sasa ni marehemu katika
shughuli za kikazi Misima.
Ni majonzi makubwa yaliyotokea leo baada ya kuwapoteza Watanzania
wenzetu, wakiwamo waandishi wawili na Afisa Uhamiaji ambao kwa pamoja
tunasikitishwa kutokana na vifo vyao vilivyotokea katika ajali hii ya
kutisha.
Mkuu wa Wilaya yeye hajaumia kwasababu gari lake lilikuwa la mbele,
ingawa ni msafara wake kwa pamoja, hivyo tumeguswa na vifo hivi
vilivyotokea katika wilaya yetu leo,” alisema.
Vifo vya waandishi hao ambao wana mchango mkubwa wilayani humo vitakuwa
ni pigo kwa Watanzania wote, wakiwamo wananchi wa Handeni ambao kwa
hakika mikono ya waandishi hao ilitumika vyema kuhabarisha umma kwenye
vyombo vyao.
Chanzo: FatherKidevu
No comments:
Post a Comment